Mourinho Azua Ugomvi Kwenye Mitandao ya Kijamii
Mashabiki wa The Blues wameonyesha hofu hiyo kupitia mitandao ya kijamii, ambapo wengi wao wanahoji maamuzi ya Jose Mourinho ambayo huenda yakamsababishia ufinyu mshambuliaji huyo kucheza mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi ya nchini Uingereza dhidi ya Arsenal.
Kwa nyakati tofauti mashabiki wa The Blues wamekuwa wakijibishana katika mitandao ya kijamii, ambapo kuna upande wanamuunga mkono Mouronho kufanya maamuzi hayo lakini wengi wao wanapinga na wanashauri meneja huyo kutokla nchini Ureno kumpumzisha Costa.
Mashabiki wa Chelsea wamekuwa na hali ya sintofahamu dhidi ya mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kutoka kwa mabingwa wa soka nchini Hispania Atletico Madrid, kwa kuhofia huenda akapata majeraha ambayo huenda yakamuweka nje kwa kipindi kirefu.
Sintofahamu hiyo inatokana na wasi wasi ulioonyeshwa na Jose Mourinho majuma mawili yaliyopita kwa kudai Diego costa anapaswa kupumzika kutokana na hali yake kutokuwa vizuri sana kufuatia majeraha yaliyokuwa yakimuandama mwishoni mwa msimu uliopita.
Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliohusu mchezo wa hii leo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon utakaochezwa nchini Ureno, meneja huyo aliweka wazi mipango ya kutarajia kumtumia Costa ambaye anaongoza kwa ufungaji wa mabao katika ligi ya nchini Uingereza.