Mwasiti aweka wazi shows zinazompa pesa nyingi zaidi

Mwimbaji wa Serebuka, Mwasiti ni mmoja kati ya wasanii wa kike ambao hawaonekani sana kwenye shows za uwanjani lakini mwenyewe anasema kuna shows zake zinazomuingizia pesa nyingi zaidi.

 “Nafikiri watu wengi hawanionagi kwenye shows za uwanjani sana lakini kuna shows zangu ambazo nikipiga mpunga napiga pesa ya maana sana (anacheka).” Mwasiti ameiambia .
“Kuna vijana wanapenda sana Zouk Rhumba huwezi amini. Na kuna wa umri fulani sasa wale wa miaka 35 kwenda juu wanapenda sana Zouk Rhumba, kwa hiyo wale huwa wana corporate shows, viongozi na nini.
“Kwa hiyo mara nyingi nafanya hizo sana kuliko zile za uwanjani ambazo wengi wanategemea kuniona, za vijana zaidi. Kibiashara iko vizuri as long as unatoa kazi ambayo wataielewa.” Ameongeza.
Mwasiti anatarajia kuachia nyimbo mbili hivi karibuni. ‘Leo’ aliomshirikisha Godzilla na ‘Kisigino’.

Popular Posts