Pearson: Kutokata Tamaa Na Kujituma, Ndio Siri Ya Kumaliza Uteja Tangu Mwaka 1985
Pearson, amesema kutokata tamaa na kujituma kwa wachezaji wake ndio ilikuwa siri kubwa ya mafanikio ya ushindi huo ambao unavunja mwiko wa kuwa kibonde wa Man Utd tangu mwaka 1985.
Amesema haikuwa kazi rahisi kwake pamoja na wachezaji wote kuamini kama wangefanikisha ushindi huo mkubwa, kutokana na uhalisia wa mchezo ulivyokuwa lakini alijikaza kisabuni na kuwahimiza vijana wake wacheze pasina na kukata tamaa kutokana na kuamini kwamba soka halina mwenyewe.
