Pellegrini Ashindwa Kujizuia Akiri Hadharani Lampard Ni Balaa
Pallegrini amelazimika kukubali hadharani umuhimu wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, baada ya kukunwa na kiwango safi ambacho alikionyesha usiku wa kuamkia hii leo wakati wa mchezo wa kombe la ligi *Capital One Cup* ambapo Man City walipambana na Sheff Wed.
Meneja huyo kutoka nchini Chile, amesema kiwango kinacho onyeshwa na Lampard kinamstaajabisha na pengine kinawastaajabisha mashabiki wengi ulimwenguni kote kutokana na umri mkubwa alionao, hivyo hana budi kusema anamkubali kwa kile anachokifanya kikosini mwake.
Amesema Lampard alicheza vyema katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo ambao ulishuhudia kikosi chake kikipata ushindi wa mabao saba kwa sifuri dhidi ya Sheffield Wednesday huku kiungo huyo akifunga mabao mawili.