Pellegrini: Msimu Wa 2013-14 Tulianza Kufungwa Na Bayern Munich

Wakati michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ikiendelea tena hii leo, mabingwa wa soka nchini Uingereza Man city hii leo watakuwa nyumbani Etihad Stadium wakipambana na AS Roma kutoka nchini Italia katika mchezo wa kundi la tano.

Man City watakuwa na kila sababu ya kutaka kujiondoa katika mawazo ya kupoteza mchezo wa awali wa kundi hilo baada ya kupoteza mbele ya mabingwa wa soka kutoka nchini Ujerumani FC Bayern Munich majuma mawili yaliyopita.
Beki wa pembeni kutoka nchini Uingereza na klabu ya AS Roma Ashely Cole amesema kikosi chao kinakwenda mjini Manchester pasi na hofu yoyote kutokana na mwenendo wao kuwa mzuri tangu mwanzoni mwa msimu wa michuano hiyo.
Cole, ambaye aliihama Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita amesema hofu kubwa itakuwa kwa wenyeji wao Man city kutokana na hitaji lao la kutaka kuwaridhisha mashabiki watakaofurika kwenye uwanja wa Etihad hii leo.
Hata hivyo meneja wa Man City Manuel Pellegrini amesema kikosi chake kipo tayari kupambana na katu hakina mshawasha wa kuelekea kwenye mpambano wa hii leo kama Ashely Cole alivyodai.
Amesema kupoteza mchezo uliopita ilikuwa kama bahati mbaya kwao na pia msimu uliopita walianza na FC Bayern Munich na walipoteza hivyo haoni sababu za kukubaliana na maneno yanayozungumzwa.

Popular Posts