Pellegrini Na Mourinho Warushiana Vijembe Baada Ya Sare Ya Moja Moja
Mabingwa wa soka nchini Uingereza Man City baada ya
kulazimisha sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Chelsea, wamewatupia
lawama wapinzani wao kwa kushindwa kucheza soka la ushindani na badala
yake waluibaki kulinda ukanda wao kwa kuhofia kipigo.
Bossi wa vijana wa Sheikh Mansoor bin Zayed bin Sultan bin Zayed bin Khalifa Al Nahyan, Manuel Luis Pellegrini Ripamonti amemlaumu mpinzani wake Jose Mourinho kutokana na mfumo wa kidhalimu alioutumia hapo jana.
Pellegrini amesema Jose Mourinho hakuwa na haja ya kuwaamuru wachezjai wake kucheza kwa kujihami muda wote kutokana na soka la sasa kuhitaji mbinu za kushindana na si kubaki langoni kwa kuhofia kufungwa.
Amesema hii ni mara ya pili kwake kuona timu inayocheza dhidi ya kikosi chake inalikaa nyuma na kulinda lango lake ambapo kwa mara ya kwanza msimu huu alikutana na kadhia hiyo alipotunishiana msuli na Stoke City ambao waliondoka Etihad Stadium na ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Amesema pamoja na yote hayo kuwakabili bado kikosi chake kilionyesha soka safi na kwake anaamini mchezo dhidi ya Chelsea huenda ukawa bora kwa msimu huu.
Jose Mourinho hakusita kumjibu Manuel Pellegrini kwa kumwambia hakwenda Etihad Stadium kwa ajili ya kuangalia Man city wanacheza vipi ama awaelekeze namna ya kucheza, zaidi ya kuhakikisha anapata matokeo ambayo yataendelea kukifanya kikosi chake kukaa kileleni.
Amesema walikwenda Etihad Stadium wakijua ni mahala pagumu, lakini walijitahidi na mwihowe wameondoka na point moja ambayo inaendelea kuwaweka kileleni kwa tofauti ya point dhidi ya Southampton wanaoshika nafasi ya pili.
Matokeo ya michezo mingine ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza iliyochezwa mwishoni mwa juma lililopita ni kwamba:
White Hart Lane:
Tottenham 0 - 1 West Brom
Goodson Park:
Everton 2 - 3 Crystal Palace