Rich Mavoko awataka wasanii kumuangalia Adam Juma 'ametutoa mbali'

Mwimbaji wa Bongo Flava, Rich Mavoko amewataka wasanii wa Tanzania kukumbuka mchago wa mtayarishaji mkongwe wa videos za muziki nchini Adam Juma pale wanapofikiria kuhusu kiasi cha kumlipa.

Akiongea Rich Mavoko ambaye anatarajia kuachia video mpya ya wimbo wake ‘Pacha Wangu’ aliyoifanya Cape Town, Afrika Kusini na kuongozwa na Adam Juma amewataka wasanii wasilalamike kuwa Adam Juma anahitaji pesa nyingi ya kufanyia video bila kukumbuka uwezo wake na mchango wake.
“Lakini tuangalie pia ametutoa wapi. Movement zake kuhusu music video Adam Juma ameitoa wapi. Tuapreciate kitu ambacho amekifanya. Mimi naweza nika-appreciate media, maDj, na wasanii wenzangu basi tuapreciate pia (Adam J) ametutoa mbali ujue.” Rich Mavoko ameiambia tovuti ya Times Fm.
Akizungumzia kuhusu video yake, ameeleza kuwa Adam Juma alisafiri na crew yake yote na alitumia vifaa vya kisasa kukamilisha kazi nzima Cape Town.
“Analipwa kawaida, analipwa vilevile tu.” Ameongeza.

Popular Posts