Rihanna kuigiza filamu ya 'James Bond'

Ripoti zilizotolewa na gazeti la Sunday Mirror zinaeleza kuwa waandaaji wa movie za Bond wamemuomba Rihanna kuigiza kama ‘Bond Girl’ kwenye filamu hizo.

Kwa mujibu wa chanzo cha Sunday Mirror, Rihanna anadaiwa kuifurahia sana offer hiyo kwa kuwa yeye pia ni shabiki mkubwa wa filamu za James Bond.
“Rihanna ni shabiki mkubwa sana wa filamu za Bond na ameipenda sana aidea ya kuonekana kwenye moja kati ya filamu hizo. Hakutaka hata kufikiria kuhusu ombi la waandaaji hao, anajua anataka kufanya.” Kilieleza chanzo hicho.
Daniel Craig ambaye anacheza uhusika wa James Bond kwa sasa atakuwa ameshampitisha Rihanna kwa kuwa aliwahi kumpendekeza kama ‘dream Bond Girl’ wake alipoambiwa kupendekeza kati ya Beyonce na Rihanna.
Filamu ya James Bond ijayo iliyopewa jina la ‘Bond 24’ iliyoongozwa na Sam Mendes inatarajiwa kutoka November 2015.

Popular Posts