Rooney Aonyesha Ushupavu Na Kurejesha Salamu Kwa Maadui Wa Man Utd

Nahodha na mshambuliaji wa klabu Man Utd, Wayne Mark Rooney ameonyesha kuwa na matarajio ya kufanya vizuri msimu huu licha ya kukabiliwa na mwenendo mbovu wa kuanza ligi kuu ya soka nchini Uingereza chini ya meneja kutoka nchini Uholanzi Louis van Gaal.

Rooney, ametoa msisitizo huo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Facebook, ambapo ameandika ana mtazamo tofauti na jinsi ambavyo watu wanavyo wachukulia Man Utd, kutokana na matokeo mabaya ya mwishoni mwa juma lililopita baada ya kufungwa na klabu ya Leicester City mabao 5-3.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameongeza kuwa kila anapowangalia wachezaji waliopo kwenye chumba cha kubadilishia nguo, anaona vipaji  ambavyo vikichanganywa na umakini wa meneja wao hana shaka kwamba klabu hiyo itapata mafanikio.
Man Utd, imekuwa haifanyi vizuri tangu mwanzoni mwa msimu huu na mpaka sasa imeshapoteza michezo miwili, kutoka sare mara mbili na kushinda mmoja.

Popular Posts