Santos Akabidhiwa Jukumu La Kuifikisha Ureno Kwenye Fainali Za Euro 2016 Ufaransa

Shirikisho la soka nchini Ureno FPF, limekamilisha mpango wa kumpa ajira kocha kutoka nchini humo Fernando Manuel Costa Santos ambaye anachukua nafasi ya Paulo Jorge Gomes Bento aliyetimuliwa kufuatia mambo kumuendea kombo wakati wa fainali za kombe la dunia.

Fernando Santos ametambulishwa rasmi kwa waandidhi wa habari na ameonyesha kuaminiwa mno na viongozi wa shirikisho la soka nchini Ureno kutokana na kazi nzuri aliyoifanya akiwa na timu ya taifa ya Ugiriki.
Mtihani wa kwanza aliopewa Santos ni kuhakikisha timu ya taifa ya Ureno inafuzu kutinga kwenye fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 ambazo zitafanyika nchini Ufaransa.
Akizungumza mara baada ya utambulisho wake kwa waandishi wa habari kocha huyo mwenye umri 59 amesema ni furaha kwake kurejea nyumbani tena kuinoa timu ambayo alikuwa anaihusudu kwa siku nyingi.
Mchezo wa kwanza ambao utashuhudia Santos akiwa kwenye benchi la timu ya taifa ya Ureno utakuwa dhdi ya taifa ya Denmark ambao umepangwa kuchezwa Oktoba 14 huko Telia Parken, mjini Copenhagen.
Mchezo huo utakuwa ni wa pili kwa timu ya taifa ya Ureno katika harakati zake za kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya.

Popular Posts