Torres Afungua Akaunti Akiwa na AC Milan Ya Italia

Mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Fernando Torres ameanza kufanya kazi yake akiwa na klabu ya AC Milan iliyomsajili kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Chelsea ya jijini London nchini Uingereza.

Torres, aliyelazimika kuondoka Chelsea kutokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi katika kikosi cha kwanza, ameanza kufanya yake akiwa na AC Milan baada ya kufunga bao lake la kwanza usiku wa kuamkia hii leo wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Italia, Sirie A dhidi ya Empoli.
Katika mchezo huo, Torres alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza baada ya kuanzishwa kama mchezaji wa akiba katika mchezo uliopita.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alifunga bao hilo kwa kichwa katika dakika ya 43, kabla ya Keisuke Honda hajafunga bao la kusawazisha katika dakika ya 58.
Mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili na hivyo kuifanya AC Milan kusogea hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ya Sirie A kwa kufikisha point Saba.

Popular Posts