Tyson amsapraiz mwendesha pikipiki aliyegongwa na gari mbele yake

Bingwa wa dunia wa zamani wa ngumi za uzito wa juu, Mike Tyson ambaye anajulikana zaidi kwa hasira na vurugu ametenda tendo jema lililomshangaza mwendesha pikipiki Ryan Chesley, aliyepata ajali wiki iliyopita, Los Vegas, Marekani.

Mwanasheria wa Ryan Chesley ameeleza kuwa mteja wake alipata ajali baada ya kugongwa na taxi  Jumanne usiku ambapo alitoka kwenye pikipiki na kuanguka chini.
Lakini alipoangalia juu baada ya mshtuko alimuona Mike Tyson aliyekuwa anapiga kelele akiwataka watu wasimguse akijaribu kumsaidia.
Mwanasheria huyo amesema mteja wake alishangaa na alihisi yuko katika dunia nyingine kabisa baada ya kumuona Tyson pale.
Chesley ambaye aliumia vibaya hasa mkono wake wa kushoto, alitumia mkono wake wa kulia kupiga picha na Tyson baada ya kupewa msaada.
Msaidizi wa Mike Tyson ameeleza kuwa Ijumaa iliyopita Mike alipokea barua iliyoandikwa kwa mkono kutoka kwa Chesley akimshukuru kwa tendo jema alilomfanyia.

Popular Posts