Van Gaal:tuna mlinzi wa kati mmoja tu
Kocha
wa machester United, Louis van Gaal amesema Manchester united ina
mlinzi wa kati mmoja tu mwenye uzoefu wakati huu kikosi hicho
kinapotarajia kukipiga na west ham katika michuano ya ligi kuu ya
England.
Marcos Rojo yuko fiti, lakini timu hiyo ina majeruhi kama Chris Smalling ana jeraha la mguu, Phil Jones ana jeraha kwenye, Jonny Evans ana jeraha la kifundo cha mguu na Tyler Blackett hatacheza mchezo huo.
Van Gaal analazimika sasa kuchukua wachezaji kwenye kikosi cha vijana ili kuziba mapengo yaliyopo kwenye timu yake.miongoni mwao ni vijana Tom Thorpe na Paddy MacNair ambao wataungana na kikosi cha kwanza cha Manchester United kwa mara ya kwanza.