Watayarishaji wa 'Homeland' waibadili Cape Town kuwa Pakistan na Washington, hutoamini kiasi walichotumia

Watayarishaji na waigizaji wote wa Series maarufu yenye mikasa ya kigaidi “Homeland”, wako Cape Town, Afrika kusini wakikamilisha msimu wa nne wa series hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

November mwaka huu, watakamilisha miezi sita wakiwa Cape Town ambapo watakuwa wamemaliza kushuti msimu huo.
Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Variety , waandaaji hao wameeleza kuwa wameweza kuibadili mitaa ya Cape Town na kuivisha taswira ya Islamabad, Kabul na Washington DC ili filamu hiyo iwe imebeba sehemu tatu zenye uhalisia.
Wakizungumzia kiasi cha pesa walichotumia hadi hivi sasa, waandaaji hao wamesema zaidi ya $100,000 (Sawa na Tsh.167, 050, 000) zimetumika kwa ajili ya magari peke yake. Sasa tengeneza picha ya majengo na vyote vitakavyoonekana!

Popular Posts