Zola Katika Mawindo Ya Tycoon Kutoka Asia Shahid Shad Khan

Gwiji wa soka wa klabu ya Chelsea, Gianfranco Zola ametajwa kwenye orodha ya mameneja wanaofikiriwa kupewa ajira ya kukinoa kikosi cha Fulhm ambacho kwa sasa hakina kiongozi wa benchi la ufundi kufuatia kufukuzwa kwa Felix Magath juma lililopita.

Jina Zola linatajwa kuwepo kwenye orodha hiyo sambamba na Chris Hughton, Tim Sherwood, Steve Clarke pamoja na meneja anaekiendesha kikosi cha The Cottagers kwa muda Kit Symons.
Zola, mwenye umri wa miaka 48, alikuwa hatarajii kuwa sehemu ya orodha ya mameneja wanaofikiriwa kupewa ajira huko Craven Cottage lakini gazeti la The Mirror limeibua taarifa hizo.
Mmiliki wa klabu ya Fulham, Shahid Shad Khan kwa sasa anaendelea kufanya vikao vya ndani kwa ndani na viongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kumpata mrithi wa Felix Magath.
Hata hivyo inaelezwa kwamba kibopa huyo kutoka barani Asia hana haraka ya kutajwa kwa meneja mpya kwa sasa kutokana na uchunguzi wa kina anaoendelea kuufanya, kwa lengo la kuhitaji mtu sahihi atakae kiongoza kikosi chake kwa muda mrefu.
Felix Magath, alifunguliwa mlango wa kutokea huko magharibi mwa London baada ya kushindwa kufikia malengo aliyowekewa na viongozi wake ya kuhakikisha anapata ushindi katika michezo kadhaa liyopangiwa.

Popular Posts