CHANGAMOTO KUBWA WENGER AKIONDOKA - GAZIDIS


Changamoto kubwa kwa Arsenal itakuwa kutafuta meneja atakayechukua nafasi ya Arsene Wenger atakapoondoka Arsenal. Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu Ivan Gazidis. Wenger, ambaye atafikisha umri wa miaka 65 Oktoba 22, alisaini mkataba wa miaka mitatu mwezi Mei. "Changamoto kubwa tutakayokabiliana nayo kama klabu, ni kipindi cha mpito kutoka kwa Arsene Wenger kwenda kwa meneja mwingine," amesema Gazidis. "Tuna meneja mzuri sana. Arsene wameiweka klabu mahala pazuri mno."
Arsenal imefuzu kucheza Klabu Bingwa Ulaya kwa miaka 17 mfululizo chini ya Wenger, na Mfaransa huyo ameiongoza Arsenal kunyakua kombe la kwanza katika kipindi cha miaka tisa mwezi Mei walipoichapa Hull City katika fainali ya Kombe la FA. Wenger aliteuliwa Septemba 1996 akiwa hafahamiki, akitokea klabu ya Grampus Eight ya Japan. Wenger kwa sasa ndiye meneja aliyedumu kwa muda mrefu katika ligi kuu ya England. Alishinda Kombe la Ligi Kuu ya England mwaka 1997-98, 2001-02, na 2003-04.
Klabu hiyo ilihama kutoka Highbury na kwenda kwenye uwanja mpya wa Emirates mwanzo wa msimu wa mwaka 2006-07, na Gazidis anaamini mapato mapya yamemsaidia Wenger kununua wachezaji kama Mesut Ozil na Alexis Sanchez waliogharimu takriban pauni milioni 77.
"Miaka mitano iliyopita ya kupanua mapato yetu ya kimataifa ya kibishara ni muhimu kwa klabu," Gazidis amesema.
"Inaturuhusu kwenda na kutafuta, mtu ambaye meneja anamtaka, kama vile Mesut Ozil, na kumnunua na pia Alexis Sanchez."
Gazidis ameongeza kusema: "Tofauti na hali ilivyokuwa miaka miwili au mitatu iliyopita, wakati tulipokuwa na changamoto ya kifedha na kupoteza wachezaji wetu wazuri, sasa tunasajili wachezaji wakubwa na kuwapa mikataba mirefu, watu kama Jack Wilshere na Aaron Ramsey."

Popular Posts