Cristiano Ronaldo Kurejea Manchester Imethibitika

Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo atarejea tena kwenye uwanja wa Old Trafford mjini Manchester mwezi ujao imethibitika hivyo.

Kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa na mashirikisho ya soka nchini Ureno pamoja na Argentina imebainika wazi kwamba mshambuliaji huyo atakuwepo uwanjani hapo kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya pande hizo mbili.
Hatua hiyo huenda ikawatuliza baadhi ya mashabiki wa Man Utd wanaohitaji kumuona Ronaldo akirejea uwanjani hapo akiwa amevaa jezi ya klabu yao baada ya kufanya hivyo miaka minane iliyopita.
Kikosi cha Ureno ambacho kwa sasa kinaongozwa na mshambuliaji huyo kama nahodha kitacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika uwanja wa Old Trafford Novemba 18 mwaka huu.
Fursa hiyo itamuwezesha Cristiano Ronaldo kurejea Old Trafford kwa mara ya pili tangu alipoondoka Man Utd mwaka 2009, na kama itakumbukwa kwa mara ya kwanza alirejea wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya miaka miwiwli iliyopita akiwa na Real Madrid.

Popular Posts