Jason Derulo aeleza sababu za kuanchana na Jordin Sparks, 'hivi sasa hatuongei'

Mwimbaji wa Talk Dirty, Jason Derulo ameeleza sababu ya kupigana kibuti na mpenzi ambaye pia ni mwimbaji Jordin Sparks kuwa ni pressure ya kutaka kufunga ndoa.

Mkali huyo wa Talk Dirty amefunguka wakati akifanya mahojiano na Ryan Seacrest Jumatatu ambapo alieleza kuwa wamekuwa wakibishana sana kuhusu suala la ndoa kiasi cha kushindwa kuelewana.
“Kulikuwa na pressure ya ndoa. Kulikuwa na ubishani mkubwa na vitu kama hivyo vilivyochukua muda katika uhusiano wetu.” Amesema Jason Derulo.
Ameeleza kuwa mnapokuwa na muda mbaya zaidi kuliko muda mzuri katika uhusiono inabidi kuachana.
Mwimbaji huyo amekiri kuwa hakuwa tayari kufunga ndoa na Jordin Sparks katika muda aliokuwa anapendekeza.
Hata hivyo, Jason Derulo ambaye alianza uhusino na Jordin mwaka 2011 alisisitiza kuwa hawakuachana kwa ugomvi lakini hivi sasa hawaongei.

Popular Posts