Luis Nani: Ninajitambua Kama Mchezaji Wa Man Utd, Nipo Hapa Kurejesha Kiwango
Nani amevieleza vyombo vya habari kwamba kusajiliwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon ni sehemu ya kutaka kumthibitishia meneja wa Man Utd Louis Van Gaal kama ana uwezo wa kuendelea kuwepo kwenye kikosi chake na si kufunguliwa milango ya kuondoka Old Trafford.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema hakuumizwa na kitendo cha kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon na ndio maana anaitumikia klabu hiyo kwa moyo wake wote.
Amesema anajua mashabiki wengi wanaamini huenda ikawa mwisho wake kucheza soka akiwa na Man Utd, lakini kwake anaamini bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo na mwishoni mwa msimu huu atarejea kwa ajili ya kuendeleza mipango ya kuisaidia klabu hiyo iliyomsajili mwaka 2007.