Mila Kunis na Ashton Kutcher wapata mtoto wa kwanza

Waigizaji maarufu, Mila Kunis na Ashton Kutcher wamemkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza wakiwa bado ni wachumba.

Vyanzo vya karibu vimeiambia TMZ kuwa Mila Kunis amejifungua mtoto wa kike, Cedars-Sinai Medical Centre, Los Angeles, Jumanne usiku.
Watu wa ndani vimeeleza kuwa wawili hao walifika hospitalini wakiwa peke yao bila msaidizi yeyote wala mtu wa familia.
Mila Kunis na Ashton Kutcher walianza uhusiano mwaka 2012 muda mfupi baada ya Kutcher kuachana na aliyekuwa mkewe wakati ho, Demi Moore. Mapema mwaka huu Kutcher alimvisha Kunis pete ya uchumba.

Popular Posts