Picha: Angalia Beckham Alivyokuwa Mwenyeji Wa Jay-Z Na Beyonce Parc des Princes, Jijini Paris


Gwiji wa soka nchini Uingereza David Beckham, usiku wa kuamkia hii leo alikuwa mwenyeji wa mwanamuziki maarufu duniani Jay-Z pamoja na mkewe Beyonce wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ulioshuhudia mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG wakipambana dhidi ya FC Barcelona huko mjini Paris.
Beckham, alionekana akiwa sambamba na mwanamuziki huyo wakati wote wa mchezo, huku wakizungumza kwa furaha wakiwa jukwaani.
Kiungo huyo ambaye alimalizia soka lake akiwa na klabu ya PSG mwaka 2013, pia aliongozana na mke wake Victoria katika mchezo huo.
Mbali na kuwa mwenyeji wa Jay-Z pamoja na mkewe Beyonce, Beckham pia alionekana akisalimiana na aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi, Patrick Kluivert pamoja na aliewahi kuwa raisi wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ambao wote walihudhuria kwenye mchezo huo.
Mpambano huo uliochezwa kwenye uwanja wa Parc des Princes, jijini Paris ulimalizika kwa wenyeji PSG kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya FC Barcelona.

Popular Posts