VAN GAAL ALIHITAJI WACHEZAJI WAPYA ASEMA FERGUSON

Photo: VAN GAAL ALIHITAJI WACHEZAJI WAPYA ASEMA FERGUSON
Meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekiri kuwa kikosi cha Man Utd kilihitaji "wimbi kubwa" la wachezaji wapya.
Ferguson alistaafu mwaka 2013, lakini meneja aliyechukua nafasi yake, David Moyes alifukuzwa kazi mwezi Aprili baada ya United kusuasua msimu uliopita na kumaliza katika nafasi ya saba, ya chini zaidi kushika katika Ligi Kuu ya England. Wachezaji sita wapya walinunuliwa kwa gharama ya pauni milioni 150, akiwemo Angel Di Maria aliyevunja rekodi ya Uingereza ya pauni milioni 59.7.
"Ilikuwa muhimu sana kwa sababu unahitaji wachezaji bora Manchester United, unahitaji wachezaji wazuri kabisa," amesema Ferguson.
Ferguson, 72, ambaye ameshinda mataji 38 katika miaka 26 akiwa meneja wa United ameiambia MUTV: "Hivyo ndivyo jinsi mchezo ulivyo sasa, gharama kama za pauni milioni 85 kwa Gareth Bale.
"Kama unaweza kutambua uwezo kama huo, unaotakiwa na Manchester United, wana uwezo wa kufanya hivyo.
"Ada kama hizo sikuwahi kuzifikia, lakini timu ilikuwa inahitaji wachezaji wapya mwaka huu." Amesema Ferguson. 

Popular Posts