Adebayor Achoshwa Na Tabia Za Mashabiki Wa Spurs
Mshambuliaji kutoka nchini Togo, na klabu ya Tottenham
Hotspurs Emmanuel Adebayor, amesema wachezaji wa klabu hiyo wanaogopa
kuchezea katika uwanja wao wa nyumbani.
Adebayor, amesema mara kadhaa mashabiki wao wamekua wakiwakejeli wanapocheza kwenye uwanja wa White Hart Lane, hali ambayo inawashusha morari na kujikuta wakifanya vibaya.
Wachezaji wa Spurs walizomewa na mashabiki wao wakati wa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita na kusababisha kichapo cha mabao mawili kwa moja walichokipata kutoka kwa Stoke City.
"Kwa sasa mimi naona itakuwa vyema kucheza katika uwanja mwingine lakini sio hapa White Hart Lane ambapo pamekua na maudhi kila kukicha, mashabiki hawatukubali na sijui kwa nini,'' Alisema Adebayor.
"Tukicheza katika viwanja vya ugenini itakuwa vyema maana kama kuzomewa tutazomewa na mahasimu wala sio mashabiki wetu.'' Aliongeza Adebayor
Tangu msimu huu wa 2014-15 ulipoanza kikosi cha Spurs tayari kimeshapoteza michezo minne kati ya sita waliyocheza katika uwanja wa nyumbani.