David Moyes Anapambana Na Pepe Mel Kusaka Ajira Hispania
Klabu ya Real Sociedad imethibitisha kuwa katika mpango wa
kumpa ajira aliyekuwa meneja wa klabu ya Man Utd, David Moyes baada ya
kumtimua Jagoba Arrasate mwishoni mwa juma lililopita.
Mwanzoni mwa juma hili klabu hiyo inayoshiriki ligi ya nchini Hispania ilihusishwa na tetesi za
kuwa mbioni kuzungumza na Moyes, lakini kwa sasa uongozi umethibitisha rasmi taarifa hizo.
Hata hivyo Moyes itamlazimu kusubiri kikao cha wakuu wa klabu hiyo kupitia wasifu wa makocha ambao anawania nao nafasi ya kuwa mkuu wa becnhi la ufundi la Real Sociadad.
Taarifa hutoka nchini Hispania zinaeleza kwamba Moyes, ameingia kwenye orodha ya mameneja wanaofikiriwa kupewa ajira klabuni hapo na siku si nyingi atakaeonekana anafaa atatangazwa.
Maneja mwingine anaowania nafasi hiyo alietajwa kwenye orodha ni aliyekua meneja wa klabu ya West Brom, Pepe Mel
.