DAVIDO KUFANYA KAZI NA DRAKE
Kwa mujibu wa Nigeria Film, Davido amesema tayari ameanza mazungumzo na
star huyo kuhusu collabo hiyo anayotarajia itakuwa kubwa.
“Nina mipango ya kufanya collabo na Drake. Ninapenda aina ya muziki wake. Itakuwa ni bomu! Kitu ambacho mashabiki wangu watafurahia. Tayari tuko kwenye mazungumzo juu ya hilo. Alisema Davido.”
Wakati Davido yuko kwenye mpango wa collabo na Drake, mpinzani wake mkubwa kwa Nigeria, Wizkid tayari amethibitisha kuwa amefanya collabo na aliyekuwa adui wa Drake, Chris Brown ambao kwa sasa wamemaliza tofauti zao na kuwa washkaji tena.