Hatimaye Kelly Rowland Apata Dume


Mwanamuziki kutoka kundi la Destiny's Child kelly Rowland amefanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume.Kwa mujbiu wa taarifa iliyotolewa kwa  vyombo vya habari kelly alijifungua mtoto huyo salama huku akiwa sambamba na mpenzi wake aitwae Tim Witherspoon.

Wawili hao walitoa taarifa kuwa wanafurahi kutangaza kuzaliwa kwa mtoto wao atakaefahamika kwa jina la Titan Jewell Witherspoon ambae amezaliwa akiwa salama sambamba na afya ya mama yake na kuongeza kuwa wanajisikia fahari kua wazazi.
huyo ni mtoto wa kwanza kwa mwanadada huyo kutoka kundi la Destiny's Child

Popular Posts