MISS TZ 2014 SITTI MTEMVU AMELIVUA RASMI TAJI HILO

Mshindi wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu, kwa hiari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu ameamua kulivua rasmi taji hilo la urembo.
Mratibu wa shindano hilo Hashimu Lundenga amesema kuwa Sitti Mtemvu ameamua kwa maamuzi yake binafsi na sio wao kama kamati ya Miss Tanzania.


"Sababu kubwa ya Sitti kulivua taji hilo ni baada ya kuchoshwwa na maneno mengi yaliyozushwa juu yake, maana pia aliitwa na RITA kwaajili ya uchunguzi zaidi hivyo ameona mambo yanazidi kuzushwa mengi hivyo ameamua kulivua taji hilo". Amesema Hashimu Lundenga

Baada ya Sitti Mtemvu kulivua taji hilo atavalishwa aliyekuwa mshindi wa pili Lilian Kamazima


Barua ya Sitti ilikuwa na maneno haya
        

“Napenda niwashukuru wale wote
waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano
haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja
na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma
shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na
wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata.
Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya
Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”Leo nalivua taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi  Mungu bado ninalo.

Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo
niliochukua.” 

Popular Posts