Moyes Apitia Mlango wa Hispania, Akabidhiwa Jukumu Zito Anoeta Stadium
Aliyekua meneja wa kikosi cha Man Utd David William Moyes,
hatimae amerejea katika tasnia ya ufundishaji soka baada ya kuwa nje ya
ulingo kwa muda wa miezi kadhaa iliyopita.
Moyes amerejea kazini baada ya kumalizana na viongozi wa klabu ya
Real Sociedad ya nchini Hispania ambayo majuma mawili yaliyopita ilimpa
mkono wa kwaheri meneja mzawa Jagoba Arrasate Elustondo.
Moyes amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utamuwezesha kutimiza malengo aliyowekewa na mabosi wake wapya ambao walionyesha kuchoshwa na matokeo ambayo wamekua wakiyapata tangu mwanzoni mwa msimu huu.
Inaaminika wazi kwamba ajira ya meneja huyo mwenye umri wa miaka 51, itakua chagizo kwa wachezaji wote klabuni hapo ambao wamekua wakijitahidi kwa namna zote kufikia malengo.
Moyes ambaye alidumu kwa muda mrefu akiwa na klabu ya Everton kabla ya kuelekea Man Utd, atafanya kazi na wachezjai wenye uwezo mkubwa huko Anoeta Stadium kama Carlos Vela, Rubén Pardo, Sergio Canales, Iñigo Martínez pamoja na kiungo mzoefu Xabi Prieto.
Rekodi ya David Moyes inaonyesha alikisimamia kikosi cha Everton katika michezo 427, akapata ushindi katika michezo 173, akapata matokeo ya sare katika michezo 123 na alipoteza michezo 131.
Kwa upande wa Man utd alikisimamia kikosi cha klabu hiyo ya Old Trafford katika michezo 34, akapata ushindi katika michezo 17, akapata matokeo ya sare katika michezo 6 na alipoteza michezo 11.
Mapema hii leo kwa saa nchini Hispania David Moyes anatarajiwa kutambulishwa kwa waandishi wa habari.