Mwanamitindo Nchini Italia Kuchezesha Ligi Ya Serial A


Mwanamitindo nchini Italia Claudia Romani ameamua kujiingiza katika kazi ya uwamuzi wa mchezo pendwa duniani mpira wa miguu baada ya kufanikiwa kushinda mtihani wa waamuzi kwa lengo la kuwa mwamuzi wa kimataifa.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 32, ameamua kuachana na mambo mengine yote ili awe mwamuzi kitu ambacho kilikuwa katika malengo yake kwa muda mrefu.
Romani amefuzu na kuingizwa katika ratiba ya michezo ya ligi kuu ya Italia Serie A na Serie B kitu ambacho sasa anajivunia.
Amekaririwa akisema
“Kukimbia uwanjani ukiwa na wachezaji wote na ukiamuru mipigo ni fursa ya kipekee.”
Kabla ya kufikia hapo haikuwahi kutokea mwamuzi mwanamke aliyeweza kuchezesha ligi kuu ya Italia Serie A kutokana na kukusa uzoefu wa kutosha.
Hivyo basi ni changamoto kwa Romani kuanza kuonekana katika ligi ya Italia.

Popular Posts