BARNES AEPUKA ADHABU



Mshambuliaji wa Burnley Ashley Barnes hatokabiliwa na adhabu yoyote kutoka kwa FA kwa jinsi alivyomkabili Nemanja Matic, katika mchezo ulioishia kwa sare ya 1-1 na Chelsea.

Barnes aliupata mpira, lakini alimkwatua Matic kwenye ugoko huku njumu zake zikiwa juu. Matic alioneshwa kadi nyekundu kwa kukasirishwa na tukio hilo na kumsukuma Barnes, ambaye hakuadhibiwa na mwamuzi. "FA inathibitisha kuwa hakuna hatua zaidi itachukuliwa kwa Ashely Barnes kwa jinsi tukio lilivyoonekana na waamuzi," kimesema chama cha soka cha England, FA. FA imetoa maelekezo kupitia twitter kuzungumzia sababu za uamuzi waliofikia.

Popular Posts