Gerrard asema Balotelli hana 'heshima'
Nahodha wa timu ya Liverpool Steven Gerrard amemshtumu mshambuliaji wa timu hiyo Mario Balotelli kwa kutokuwa na heshima baada ya kuchukua mkwaju wa penalti wa bao la ushindi dhidi ya Besikitas badala ya nahodha Jordan Henderson.
Balotelli alifunga penalti hiyo siku ya ahamisi katika mechi ya ligi ya Yuropa iliochezwa katika uwanja wa Anfield ili kupata ushindi wa 1-0.
Hatua hiyo inajiri baada ya Balotelli kubishana na nahodha Henderson na mshambuliaji Daniel Sturridge kuhusu ni nani angefaa kupiga mkwaju huo.
Gerrard alisema:Henderson ndio nahodha na Balotelli alimuonyesha madharau.