Majasusi wa Uingereza na Marekani walikiuka sheria na kudakua kampuni inayotengeneza kifaa kinachotumika kwa simu za mkononi yaani ''Sim Card''Tovuti moja ya habari za teknolojia imeripoti huko Marekani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo Majasusi hao waliiba mfumo na data inayowaruhusu kusikiza mawasiliano mbali na kujua alipo mmiliki wa simu hiyo lengwa.
Habari hiyo ambayo chanzo chake inasemekana kuwa ni aliyekuwa mfanyikazi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, Edward Snowden
inaziwezesha mashirika hayo mawili ya kijasusi kudukua mamilioni ya simu za mkononi kote duniani.
Kampuni hiyo lengwa Gemalto imesema kuwa imeshtuliwa na madai hayo na kuwa inayachunguza kwa kina.
Kampuni hiyo inahudumia mataifa 85 kupitia mashirika 40.
Aidha kampuni hiyo inazihudumia makampuni 450 kote duniani.



Takriban wateja wa makampuni 450 za simu kote duniani wanadukuliwa na majasusi wa Marekani na Uingereza

Habari hiyo inaeleza kuwa wateja wa kampuni ya simu ya AT&T, T-Mobile, Verizon, Sprint na kampuni zingine 450 kote duniani zimeathirika.
Taarifa hiyo inasema kuwa udukuzi huo ulifanyika tangu mwaka wa 2010.
Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Washington Marekani Naomi Grimley anasema wizi huo umewawezesha majasusi wa Marekani na Uingereza
kudukua simu za wateja mataifa ya kigeni na hata kunakili jumbe zinazotumwa kutoka kwa simu hizo bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa serikali ama makampuni ya simu.

Popular Posts