ACT Kuzinduliwa Kwa Bashasha Jijini Dar
Chama Kipya kwenye medani za siasa nchini Tanzania ACT kinatarajiwa kufanya uzinduzi wa kishindo jijini Dares salaam Machi 27-29 mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha Habari kutoka ndani ya chama hicho kimeeleza kwamba mtoto wa Rais wa Kwanza wa Ghana, Dk. Kwame Nkurumah, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha CPP, Samia Nkrumah, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Mara baada ya uzinduzi huo chama hicho kitafanya mkutano mkuu wa Kwanza ambapo utahusisha ajenda kuu ya kuwapata viongozi wa kitaifa, wakiwemo Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na manaibu wake.
Chanzo hicho kimesisitiza kuwa katika uzinduzi huo watanzania watawafahamu wanasiasa mahiri na maarufu waliopo ndani ya chama hicho ambao hawajajulikana.
Viongozi wengine watakao shiriki uzinduzi huo ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi. mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali.