Angalia Suarez Alichowafanyia Real Madrid Usiku wa Kuamkia Leo
Usiku wa kuamkia hii leo palipigwa mtanange wa El Classico katika uwanja wa Camp Nou ambapo wenyeji FC Barcelona walikua wakijiuliza mbele ya Real Madrid waliokua wamefunga safari kutoka mjini Madrid kwenda kuzisaka point tatu muhimu mjini Barcelona.
Barcelona 2 - 1 Real Madrid
19' Jeremy Mathieu (assist) Lionel Messi
56' Luis Suarez (assist) Daniel Alves 2 - 1
31’ Cristiano Ronaldo (assist) Karim Benzema
Mshambuliaji Luis Suarez akishangilia sambamba na wachezaji wenzake wa Barcelona baada ya kufunga bao la ushindi.
Suarez akipiga mpira uliozaa bao kati kati ya mabeki wa Real Madrid Pepe pamoja na Sergio Ramos.
Wachezaji wa Real Madrid wakionyesha kukatishwa tamaa baada ya kufungwa bao la pili.
Lionel Messi akiwa Katika harakati za kuipangua ngome ya wapinzani.
Jeremy Mathieu aliifungia FC Barcelona bao la kuongoza katika dakika ya 19.
Mlinda mlango wa Real Madrid, Iker Casillas akiutazama mpira uliotinga nyavuni baada ya kupuigwa kichwa na Jeremy Mathieu.
Ronaldo akiwa katika purukushani dhidi ya ngome ya FC Barcelona kabla ya kuifungia Real Madrid bao la kusawazisha.
Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la kusawazisha na kumuacha mlinda mlango wa FC Barcelona Claudio Bravo akijiuluza.
Ronaldo akipongezwa na Toni Kroos pamoja na Dani Carvajal baada ya kuisawazishia Real Madrid.
Mashabiki 95,000 walijitokeza kwenye uwanja wa Nou Camp kushuhudia kipute cha Real Madrid na FC Barcelona.
Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya nchini Hispania iliyochezwa jana ni kwamba:
Deportivo de La Coruna 0 - 0 Espanyol
Villarreal 0 - 2 Sevilla
Real Sociedad 3 - 1 Cordoba