Askofu wa pili mwanamke ateuliwa
Kanisa la Kianglikana nchini Uingereza limemteua Askofu wake wa pili mwanamke, Canon Alison White, ambaye mumewe Frank, tayari ni Askofu.
Canon White atakuwa naibu Askofu katika Jimbo la Hull, na mumewe ni Naibu askofu wa Newcastle.
Kwa wakati huu Alison ni msimamizi wa parokia katika Riding Mill katika Jimbo la Northumpland.
Askofu huyo na mumewe ni kundi la kwanza la mtu na mumewe kuwa wote maaskofu.
Mwandishi wetu wa maswala ya Kidini Carolyne Wyatt ametuandalia ripoti ifuatayo inavyosimuliwa na Jamhuri Mwavyombo)
Canon Alison White kwa wakati huu ni msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu James katika Northumberland, na ni mke wa kaimu Askofu wa Newcastle, Frank White.
Alitawazwa kuwa deacon mwaka 1987 na akawa kasisi mnamo mwaka 1994.
Askofu Frank White ni kaimu Askofu wa NewCastle na mfanyakazi wa zamani wa huduma za kijamii na ni shabiki mkubwa wa timu ya kandanda ya New Castle United.
Askofu mtarajiwa Alison White anasema kuwa na maaskofu wawili katika familia ni changamoto kubwa lakini akahakikishia waumini kuwa wataendelea na kazi yao kikamilifu kutokana na ujuzi wa ndoa ya zaidi ya miaka 30.