Australia mabingwa wa Kriketi

Australia iliishinda nguvu New Zealand na hivyobasi kuibuka mshindi wa kombe la dunia la mchezo wa Kriketi kwa mara ya tano katika uwanja wa Kriketi mjini Melbourne.

New Zealand ilimpoteza nahodha wake mwenye ushawishi mkubwa Brendon McCullum wakati wa mpira wa tano kabla ya kutolewa kwa mikimbio 183.
Grant Elliot alikuwa na mikimbio 83 huku Mitchel Starc ,Mitchel Johnson na James Faulkner wakijigawia wiketi 8.
Australia haikusumbuliwa wakijipatia wiketi ya 7 katika overs 33.1 huku nahodha Michael Clarke akifunga 74 naye Steve Smith akipata 56 bila ya kutolewa.

Popular Posts