Casillas: Buffon Ni Kivuli Cha Uvumilivu Na Mafanikio Yangu
Kwa mara ya kwanza mlinda mlango wa klabu bingwa duniani Real Madrid Iker Casillas Fernández ametoa siri ya msukumo wa mafanikio aliyoyapata tangu akiwa mdogo akifundwa mchezo wa soka akiwa na klabu hiyo yenye mafanikio mjini Madrid.
Casillas amesema siri kubwa ya mafanikio yake yametokana na mlinga mkongwe wa klabu bingwa nchini Italia Juventus Gianluigi "Gigi" Buffon ambaye alimtumia kwama kigezo cha kukaa langoni tangu akiwa na umri mdogo.
Casillas ambaye kwa miaka miwili iliyopita alionekana kushuka kiwango akiwa na klabu yake ya Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya Hispania amesema alijifunza mengi kutoka kwa Buffon na alitamani siku moja kuwa kama mlinda mlango huyo wa Italia ambaye amedumu katika soka tangu mwaka 1995 akiwa na klabu ya Parma.
Amesema amepitia mengi ambayo yalikaribia kumkatisha tamaa, lakini alijifariji kwa kumtazama na kumfikiria Buffon ambaye aliwahi kupitia madhila kama yaliyomsibu na hatimae alijipa moyo na kufikia hatua ya kurejesha heshima ya kukaa langoni kama mlinda mlango namba moja wa Real Madrid pamoja na timu ya taifa.
Hata hivyo uchunguzi wa kumbu kumbu unaonyesha Casillas mwenye umri wa miaka 33 anashabihiana na Gigi Buffon mwenye umri wa miaka 37 katika idadi ya michezo waliyocheza mpaka sasa ambayo inakadiriwa kufikia 300 kwa kila mmoja.
Iker Casillas Fernández alianza kuitumikia Real Madrid tangu akiwa na umri miaka tisa na kwa vipindi tofauti alipandishwa madaraja kwa kuzitumikia timu za vijana za klabu hiyo mpaka alipofikia hatua ya kuaminiwa na kupewa nafasi ya kuitumikia timu ya wakubwa mwaka 1999 ambapo alikuwa na miaka 18.