Falcao ataka kuchezeshwa kila mara
Mshambuliaji wa Manchester United Radamel Falcao amesema kwamba amekuwa akipokea maombi kutoka vilabu tofauti huku akitafuta kilabu ambayo anaweza kuichezea kila mara.
Mshambuliaji huyo wa miaka 29 amefunga mabao manne baada ya kucheza mara 22 tangu ajiunge na kilabu hiyo kutoka Monaco kwa mkopo.
Lakini hajaanza mechi yoyote tangu ushindi wa 2-0 dhidi ya Sunderland mnamo mwezi februari 28.
''Nataka mahali ambapo nitaendelea na nitaenda kucheza kila mara'',Falcao aliiambia runinga ya Colombia Win sports.
Mchezaji huyo wa zamani wa Porto na Atletico Madrid aliongezea:''Maombi yanakuja kutoka kila kona kwa hivyo nafaa kutulia ili watu wengine kuliangazia swala hili''.