Jaji Warioba Amtaja Raisi Wa Awamu Ya Tano
Aliyekua waziri mkuu wakati wa serikali ya awamu ya kwanza, Jaji Joseph Warioba amesema rais ajaye anastahili kuwa mzalendo, muadilifu na dira ya kuliongoza taifa.
Jaji warioba alisema “Rais anapaswa kujua matatizo ya Watanzania, awe mzalendo, mwadilifu na anapaswa pia kujua atafanya nini ili kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta za afya na uchumi,”.
Kauli kama hizo ziliwahi kutolewa na viongozi wengine kadhaa ambao nao walitaja sifa za rais ajaye, akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dk Hassy Kitine, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Mwanasiasa mkongwe Cleopa Msuya, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk Emmanuel Nchimbi.