Kala Jeremiah Awarudisha Wasanii Kwenye Mstari
Mkali wa muziki wa kizazi kipya, Kala Jeremiah amewaasa wasanii wezake kutambua kwamba muziki siyo anasa, una kazi ya kuielimisha jamii.
Amesema baadhi ya wasanii wamejiingiza kwenye vitendo visivyofaa, kama kutumia dawa za kulevya na mambo mengine.
Jeremiah alisema kazi ya muziki ni kuelimisha na kuiburudisha jamii.
Alisema haipaswi kufanya mambo maovu, kwa kutumia mwavuli wa muziki.
“Muziki ni kazi kwa wasanii, kama sisi ambao tunautegemea, kwa hiyo baadhi ya watu wanataka kuuharibu muonekano huo.”