Kidunda: Matumla Atamchapa Mchina


Bondia wa ngumi za ridhaa nchini Selemani Kidunda anampa nafasi kubwa ya ushindi Mohamed Matumla kuelekea mpambano la kuwania ubingwa wa WBF dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini China Wang Xin Hua, lililopangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kidunda ambaye aliiwakiklisha vyema Tanzania katika michuano ya Olympic licha ya kutokutwaa medani mwaka 2012, alisema umahiri na kiwango kizuri cha Matumla unampa nafasi ya kuamini bondia huyo chipukizi hatokua na cha kupoteza ulingoni dhidi ya mpinzani wake.
“Pamoja na pambano hilo kutarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na mkanda wanaouwania mabondia hao lakini mimi nampa nafasi Muddy ya kuibuka kidedea,” alisema Kidunda.
Mshindi wa pambano hilo la kuwania mkanda wa dunia unaotambuliwa na shirikisho la ngumi za kulipwa (WBF) la uzani wa Super Bantam la raundi 12, atakwenda nchini Marekani kupambana kwenye michezo ya utangulizi kabla ya magwiji Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hawajashikishana adabu May mbili mwaka huu.
Tayari bondia kutoka nchiini China Wang Xin Hua, ameshawasili jijini Dar es salaam tangu juzi na ameahidi kushinda.

Popular Posts