Kutafuna ni haramu nchi hii
Wengi wanamkumbuka kiongozi muanzilishi wa Singapore Lee Kuan Yew,aliyeaga dunia jumatatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 91.
Hata hivyo wengi wetu ambao hatuzuru Singapore hatujui anachosifiwa kiongozi huyo ila tu sifa kedekede anazolimbikizwa katika vyombo vya habari.
Hata hivyo mojawepo ya sifa hizo ni usafi.
Kiongozi huyo aliyeongoza kisiwa cha Singapore punde kilipopata uhuru wake yapata miaka 50 hivi iliyopita alipenda taifa hilo ambalo kimsingi ilikuwa ni
bandari igeuke na kuwa taifa huru linajitegemeakiuchumi.
Na si Hayo tu Lee Yew alitaka raia wa Singapore kujivunia taifa lao japo lilikuwa changa kiuchumi ikilinganishwa na jirani zake India China Japan na Korea.
Hata ilipowadia zamu ya ustaarabu na usafi , Lee aliharamisha utafunaji wa ubani , na pipi zilizokuwa na kiungo kama raba kisa na maana ?
Yew alichukia sana watu waliotafuna ubani kisha wanatupa mabaki yake sakafuni pindi utamu wake unapokwisha.
Shinikizo la watu lilimfanya kuruhusu utafunaji wa ubani mwaka wa 1992 kwa muda kulingana naye kwa sababu vyombo vya habari vya kigeni vilikuwa
vinaangazia tu marufuku yake na kuwa watu walikuwa wanatandikwa viboko kwa makosa madogo madogo kama vile kutupa taka kukojoa hovio kutema
makohozi na makosa mengine kama hayo.
Marufuku hiyo ni moja ya maswala yanayangaziwa kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wageni katika taifa hilo lililoshamiri katika ukuaji wake wa kasi wa uchumi na pato la nchi duniani.
Nichini Singapore, ni hatia kutembea ovyo,kuandika ukutani ,kutema makohozi kukojoa sehemu yeyote ile ila chooni.
Ukishatumia choo ni sharti umwage maji la sivyo utashtakiwa.
Hatua iliyopiga katika kipindi cha uhuru wake (tangu mwaka wa 1965) hadi sasa unazidi mataifa mengi yaliyokuwa na uwezo na rasili mali inayoizidi.
Chini ya uongozi wake Singapore ilikuwa inayazidi mataifa yaliyostawi kwa usafi wa miji na mazingira kwa jumla .
Lee ambaye alisomea chuo kikuu cha Camridge nchini Uingereza aliwalazimu raiya wa Singapore kutekeleza hali ya juu ya usafi.
Kulingana na rais Yew watu ambao walidai kuwa hawawezi kufikiria bila ya kutafuna tafuna aliwashauiri kutafuna ndizi.
LKY alisema kuwa japo wanakejeliwa kuwa'' taifa linaloshikilia kukutu usafi wa mazingira kama vile yaya na mtoto''
Singapore ilikuwa inafululiza katika ustawi wa kiuchumi bila ya kujali kejeli na matusi kuwa alikuwa ni dikteta.
Lee aliwadharau sana watu walikuwa wakitafuna ubani na pipi akisema kuwa wengi wao walikuwa watundu.
LKW alidai kuwa milango ya treni za umeme zilikuwa zinakwama kwa sababu mabaki ya ubani yalikuwa yanafichwa nyuma ya milango na hivyo kusababisha
kucheleweshwa kwa usafiri wa watu wenye bidii na ari ya kufika makazini mapema.
LKW alikerwa sana na tabia hiyo ndiposa akaamrisha imegwe marufuku kutokana na kinyaa na kero kwa hali ya usafiri na usafi wa Singapore.
Tafakari hayo ya LKW ,je yanawezekana katika mataifa yetu ya Afrika ?