Mkahawa wa Kichina hauruhusu raia weusi

Mkahawa wa kichina umezua mjadala mkali nchini Kenya baada ya kuweka sheria zinazowazuia wakenya weusi kungia baada ya
saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa wasimamizi wa mkahawa huo ulioko kwenye mtaa wa kifahari wa Kilimani sheria hiyo kali inatokana na tukio la uvamizi mwaka uliopita.
Wasimamizi wanadai kuwa genge la majambazi ''weusi'' waliokuwa wamejihami kwa bunduki za rashasha waliingia katika mkahawa huo wakisingizia kuwa wateja kabla ya kuwapora wateja na wamiliki wa mkahawa huo.
Sheria hiyo kali inawaruhusu watu weusi ambao wameandamana na mdhamini wa kichina ,mhindi,ama mzungu Kuingia ndani baada ya saa kumi na moja jioni.
Afisa wa uhusiano mwema katika mkahawa huo Ms Esther Zhao, amesema kuwa hawaoni haya kuhusu sheria hiyo ambayo wanaharakati nchini Kenya wandai ya kibaguzi kwa misingi ya rangi katia taifa huru la kiafrika kwa sababu ''watu weusi wanahatarisha maisha ya wateja wao wachina''.
Afisa anayewakilisha maswala ya raiya nchini Kenya ,Bwana Otiende Amollo,amesema kuwa sheria hiyo ni kinyume cha sheria na kuwa inakiuka uhuru wa wakenya kwa misingi ya rangi jinsia na kabila.
Kinaya ni kwamba waafrika wachache wenye uwezo mkubwa na ushawishi serikalini wanasemekana kuingia katika mkahawa huo hata baada ya saa kumi na moja.
Msemaji wa ''The Chinese Restaurant'' anasema kuwa waafrika wachache mno wanaruhusiwa kwa sababu ni ''waaminifu''.
'' kwa hakika Ni vigumu sana kwetu kubaini yupi kati ya wateja wetu ni Al shabab au la''
Kuwa mwaminifu Mwafrika anastahili kuwa na uwezo wa kufuja dola 215 katika kila kikao ndani ya mkahawa huo.
Bi Zhao anasema kuwa ''wateja wao wamefurahia sheria hiyo kali dhidi ya watu weusi'' ''Wanatutarajia sisi kama wamiliki wa mkahawa huu kuwahakikishia usalama wao''.
'' kwa hakika Ni vigumu sana kwetu kubaini yupi kati ya wateja wetu ni Al shabab au la''
''Swala la wezi na majambazi pia linatusumbua sana ', ndiyo sababu haswa ya wamiliki kuamrisha raiya yeyote mweusi asiruhusiwe kuingi mle hata akiwa na senti kivipi, kwa sababu haijandikwa usoni yupi ni mwizi na yupi si mhalifu''
''Watu weusi 6 waliingia humu na kupora zaidi ya dola elfu 6 na mia tano'' alisema bi Zhao.
VITISHO VYA AL-SHABAAB
Kulingana na bi Zhao ubalozi wa Uchina uliwatahadharisha raia wao dhidi ya tishio la mashambulizi ya kundi la Al Shaabab.
Watu weusi ni hatari kwa wateja wetu
Bwana Amollo, amesema kuwa sheria hiyo inapaswa kutupiliwa mbali kwani inawafanya watu weusi kuonekana kuwa ni majambazi wote.
Aliwashauri wateja weusi waliokatazwa kuingia katika mkahawa huo wanapaswa kuishtaki kwa ubaguzi wa rangi.
Aidha ameitaka tume ya kupigania haki za kibinadamu kuishtaki mkahawa huo kwa ubaguzi wa rangi mbali na kukiuka maadili ya mtagusano wa kijamii kama ilivyoratibiwa katika katiba ya Kenya.

Popular Posts