Mwana miereka afariki katika pigano
Mwana miereka mmoja wa Mexico alifariki baada ya kupigwa ngumi katika shingo ndani ya ukumbi wa miereka.
Pedro Aguayo Ramirez mwenye umri wa miaka 35 anayejulikana kama Hijo del Perro Aguayo alianguka na kupoteza fahamu katika kamba ndani ya ukumbi wa miereka baada ya kupigwa teke na mpinzani wake Oscar Gutierrez anayejulikana kama Rey Mysterio junior,kulingana na kanda ya video ya pigano hilo ilillofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Tijuan.
Pigano hilo liliendelea kwa dakika mbili kabla ya mashabiki na refa kugundua kuwa Aguayo alikuwa amepata jereha baya na hivyobasi kuanza kumshughulikia.
''Alipelekwa katia hopsitali jirani na kufariki'',alisema Raul Gutierez wa afisi ya mashtaka ya Baja mjini California.
''Sina la kusema kufuatia kisa hiki cha kushangaza'',Joaquin Roldan ,ambaye ni mkurugenzi wa shirikisho la miereka la AAA alisema katika mtando wa twitter.
''Rambirambi natizituma kwa familia ya Aguayo''.