Mwana wa Whitney aondoshwa hospitalini

Mwana wa aliyekuwa mwanamuziki wa 'rhythm n blues' marehemu Whitney Houston Bobbi Kristina Brown ameondoshwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Emory na sasa yuko katika nyumba ya kurekebishia tabia katika jimbo la Atlanta,lakini uhaimisho huo sio ishara kwamba hali yake inaimarika.

Bobby Kristina alihamishwa hadi katika kituo hicho siku ya alhamisi baada ya madaktari wa hospitali ya Emory kujaribu tena kuona iwapo anaweza kupumua bila kutumia mashine.
Hatahivyo hakuweza kupumua na inadaiwa kuwa madaktari wanasema bado hajapata fahamu.
Bobby Brown na Pat Houston walisaidia katika kubeba mizigo ya Bobby Christina kutoka hospitali hiyo hadi kituo hicho cha kurekebishia tabia ambacho kinadaiwa kuwa kizuri katika uangalizi wa wagonjwa wa mda mrefu.
Inadaiwa kuwa Bobby Brown ambaye ni babaake Bobby Kristina ana imani kwamba mwanawe atapata fahamu.

Popular Posts