Pombe Yatajwa Kuwa Adui Wa Kijana Wa Kitanzania
Vijana wametajwa kuwa waathirika wakubwa wa magonjwa ya Kifua kikuu, Ukimwi, Kansa pamoja na ajali kutokana na matumizi ya pombe kwa kiwango cha juu na kutokuwepo kwa sera ya matumizi ya pombe.
Wakizungumza katika semina ya wadau wa masula ya afya jijini Dar es Salaam wakati wa kuwasilisha taarifa za Utafiti uliofanya na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR),uliofanywa katika Mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza ambapo Watafiti wa Taasisi hiyo wamesema kuwa matumizi ya pombe nchini yako katika kiwango cha juu na kusababisha magonjwa kuchangiwa na matumizi hayo.
Mtafiti wa NIMR Mwanza Dokta Said Kapiga amesema kuwa baada ya kufanya utafiti wamegundua kuwa yapo madhara na ongezeko la wagonjwa ambao wanatokana na matumizi ya pombe pamoja na mabadiliko mengine ya kimaisha chanzo kikubwa ni matumizi ya pombe.
Aidha Mtafiti wa Sayansi ya Jamii wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu –Kituo cha Mwanza (NIMR), Dokta Haika Osaki amesema katika utafiti wa pombe zilizo kwenye mifuko (Viroba) zinanyweka kwa kiwango cha juu na watumiaji ni vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa magonjwa kutokana na kutumia pombe.
Utafiti huo ulihusisha vijana kuanzia Miaka 15-24.