Seneta Atangaza Kumrithi Obama

Seneta Ted Cruz wa jimbo la Texas amekuwa mtu wa kwanza kutangaza kugombea urais kupitia kwenye chama cha Republican katika uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika mwaka 2016 nchini Marekani.

Seneta Ted Cruz alitangaza kuwa atagombea kiti cha urais kupitia katika chama chake wakati alipokuwa anatoa hotuba kwenye Chuo Kikuu cha Liberty, Virginia nchini humo.
Alisema“Ninagombea uraisi na nina matumaini ya kupokea msaada wenu.” Na ameahidi kuwa endapo atachaguliwa ataondoa mipango yote ya rais wa sasa Barack Obama.

Popular Posts