TANZIA: ABDUL BONGE AFARIKI DUNIA
Abdul Bonge enzi za uhai wake.
ALIYEWAHI kuwa Meneja wa wasanii na mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Chanzo cha kifo cha Abdul Bonge bado hakijafahamika ila msiba upo Manzese Tip Top.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN