Upigaji busu hadharani wapigwa marufuku
Kijiji kimoja nchini India kilichopo katika jimbo la kusini magharibi kimepiga marufuku upigaji busu wa hadharani na tabia nyengine mbaya.
Bunge la kijiji hicho kwa jina Salvador -de Mundo lililopo kilomita maili nane kutoka kazkazini mwa mji mkuu wa Goa Panaji,lilipitisha sheria hiyo kwa wingi likiwaonya watu wanaozuru eneo hilo dhidi ya vitendo kama hivyo.
''Tumeidhinisha sheria hii kufuatia malalamishi kutoka kwa wakaazi kuhusu wapenzi wanaopigana busu hadharani'',.Hii ndio hatua ya kipekee ambayo itaweza kukabiliana na tatizo hilo'',naibu chifu wa kiji hicho Reena Fernandes aliambia AFP.
Hatahivyo hakusema ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya wakiukaji wa sheria hiyo.