Waafrika Kufungiwa Milango Ya Soka Uingereza
Chama cha soka nchini England FA, kinakusudia kuandaa sheria itakayo punguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa Ulaya watakaosajiliwa katika klabu zinazoshiriki ligi za nchini humo.
Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke amesema ligi kuu ya soka nchini England ipo kwenye hatari ya kutowasaidia wachezaji wazawa na huenda wakapoteza vipaji vya wachezaji wanaotoka nje.
Katika mpango huo FA wataweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji waliokulia nchini humo.
England wamejizatiti kufanya mikakati hiyo kwa lengo la kuipa nguvu timu ya taifa ya England ambayo imekua haifanyi vizuri katika michuano mbali mbali ya kimataifa, ambapo kwa mara ya mwisho walitwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 1966.